# | aym | swa |
---|
1 | Tanzania: markanx swahili arut yatichasxäni janiw inglés arutx yatichasxaniti | Wanafunzi Nchini Tanzania Kufundishwa kwa Lugha ya Kiswahili, si Kiingereza |
2 | Escolares en Arusha, Tanzania. | Watoto wa shule mkoani Arusha, Tanzania. |
3 | Foto por el usuario de Flickr Colin J. | Picha imetolewa na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Colin J. |
4 | McMechan, bajo licencia CC. | McMechan kwa leseni ya Creative Commons. |
5 | Tanzania markax nayraruw ñä sartañampiski, inglés aru qhipar jaytxañataki kunalaykutix markapachanx swahili tayka aru yatiqañ utanakan yatichasxäni. | Tanzania iko tayari sasa kufanya mabadiliko ya historia kwa kuachana na lugha ya Kiingereza na kuanza kutumia rasmi Kiswahili kama lugha ya kujifunzia na kufundishia katika shule za nchi hiyo. |
6 | Jakayakikwete marka irpirix machaq sistema educativo apsuwayi ,tunka kimsani uru anata phaxsina aka 2015 marana, programa de desarrollo National Vision 2025 wakichäwiparjama ukhamarakiw educación básica churasini 7-11marani wawanakaru, ukat primaria ukhamarak secundaria yatiqirinakatakix inakiniw yatichäwixa, ukampirus wawanakatakix janiw yant'äwinakax mara tukuyanx utxaniti. | Sera mpya ya elimu iliyozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mnamo Februari 13, 2015, inayokwenda sambamba na Mpango wa Taifa Kuelekea 2025 inarefusha elimu za msingi kutoka miaka saba ya sasa mpaka miaka 11, na kuifanya elimu hiyo kuwa bure ikiwa ni pamoja na kuondoa mtihani wa taifa kwa wahitimu wa elimu ya msingi kuingia sekondari. |
7 | Sasispaw jichhapiniw Africa markanx q'alpach yatiqirinakarux tayka arut yatichasispa, jani ukhama lengua extranjera uka arutak yatichatazkaspati. | Hatua hii inaonekana kuwa mojawapo ya maamuzi ya kwanza kwamba nchi ya Afrika inaamua kufundisha wanafunzi wake kwa ngazi zote kwa kutumia lugha ya ki-Afrika badala ya lugha za kigeni. |
8 | Mä aruskipäwinx aru turkakipaw utjatapatx, Atetaulwa Ngatara, director adjunto de políticas del Ministerio de educación ukat Formacion profesional tuqinkirix siwa inglés arutx yatichasiskakiniw, yatiqirinak sum yatiqapxañapataki, ukampirus janiw munaskiti q'alpach materianak inglés arut yatichasiñapaxa. | Akitoa maoni yake kuhusu mabadiliko ya lugha, Atetaulwa Ngatara, naibu mkurugenzi wa sera katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, alisema Kiingereza kitaendelea kufundishwa kama lugha, na kwamba wanafunzi kujifunza Kiingereza haitamaanisha kuwa ni lazima masomo yote yafundishwe kwa lugha hiyo. |
9 | Mä artículo qillqt'atanx aka cambio de política utjatapatx Facebook tuqiruw apkatatana Oliver Stegen uka jaqixa, jupasti asesor lingüístico de la organización sin fines de lugro de desarrollo del idioma tuqinkiriwa SIL International, jupax alemán markatawa, ukhamarakiw swahili aru arst'asirirakiwa, jupasti akham kunayman arunak uñist'ayawayaraki. | Makala kuhusu mabadiliko hayo ya sera iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook naOliver Stegen, ambaye ni mzungumzaji wa Kiswahili mwenye asili ya Ujerumani na mshauri wa lugha wa shirika lisilo la kibiashara linaloshughulika na ukuzaji wa lugha SIL International, iliibua hisia mchanganyiko. Nancy Petruzzi Maurer alitania kwa salamu ya Kiingereza iliyokosewa: |
10 | Nancy Petruzzi Maurer sawkasiwayarakiw: | “Goood mauning teacha!” |
11 | Nuncamás “Gooodmauningteacha!” | Hakuna zaidi |
12 | Janipiniw juk'ampx Gooodmauningteacha sasa. Paul A Kijuuarst'awayiw swahili aruta inglés arux yatiqirinakarux robots ukaruw tukutawayi sasa: | Paul A Kijuu alitoa maoni kwa Kiswahili akisema kwamba Kiingereza kimegeuza tabaka la wasomi kuwa maroboti: |
13 | Nayax siristwa, Oliver Stegen juparux kusakiw aka turkakipäwixa. | Kwa upande wangu, Oliver Stegen mimi naona hii ni hatua nzuri sana. |
14 | Yatichasiñapaw kawkir aruts yatipki uka aruta. | Shida yetu ni kulalamika. |
15 | Inglés arux janiw yanapt'kistuti ñakixay ma robotxama tukuystuxa. | Elimu inapaswa itolewe kwa lugha inayoeleweka kwa mtumiaji. |
16 | Yatiqat markachirinakax janiw lup'ipkiti ñakijay jan yatipkchitix kuntix yatiqapkan ukxa. | Kiingereza hakitusaidii zaidi ya kutufanya maroboti. Wasomi wetu hawafikiri kwa kujitegemea kwa sababu hakuna walichojifunza wanachokielewa. |
17 | Vera Wilhelmsen jupasti sarakiw janiw munaskiti taqini universidad tuqiru sarañapaxa, ukampirus taqiniw sum yatichhutäpxañapa: | Vera Wilhelmsen alibainisha kwamba ingawa si kila mtu anahitaji kufika Chuo Kikuu lakini kila mmoja anastahili elimu bora ya msingi: |
18 | Siristwa wali kusaniwa aka yatichäwimpixa ñakijay taqini kust'apchinixa. kunatix janiw taqini secundari a yatiqawkamax puripkiti ,ukampirus yaqhipanakax janiw tukuyañkamas puripkiti. | Ninadhani ni muhimu kutafakari aina gani ya elimu ya msingi itawanufaisha watu wengi. Ni bayana kwamba mpaka leo hii si watu wengi wanafanikiwa kufika sekondari, na ni wachache sana wanahitimu elimu hiyo. |
19 | Ukhamarakiw problema-nipxaniwa ñakixay jani yatiqirinaka ni yatichirinakax wakicht'atapkiti inglés arut swahili aruru turkakipañatakixa. | Kuna tatizo pale ambapo si wanafunzi wala walimu wameandaliwa kubadilika kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza katika shule ya Sekondari. |
20 | Ukampirus yatiñasawa ukat mistsuña, nayax wali kusa sasaw lup'ta. | Ni kweli, tunapaswa kutazama athari zake, lakini ninaamini hii ni hatua nzuri ya mafanikio. |
21 | Ñakixay jan munaskchitix taqin universidad tuqiru sarañapaxa, ukampirus taqiniw suma yatichatañ munapxixa! | Si lazima kila mmoja afike Chuo Kikuu, lakini raia wote wanastahili elimu bora ya msingi! |
22 | Ukampirus janiw taqini uka amtampipkiti. | Hata hivyo, si kila mmoja aliafiki mfumo huo mpya wa elimu. |
23 | Steve Nicolleseñaló jupax sarakiw : | Steve Nicolle alibainisha uwezekano wa athari ya sera hiyo mpya ya elimu: |
24 | Escuelas privadas uka yatiqaw utanakanx matricula irxatayasipxani ,ñakijay inglés arut yatichaskakchixa. | Ninahisi athari ya sera hii itakuwa kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi katika shule binafsi ambazo zinaendelea kufundisha kwa Kiingereza. |
25 | Ukampirus amuyapxam político-nakax yatiqañ utanak jist'arasipxani akat nayraruxa sasaw arst'awayi. ! | Chunguzeni sana mtaona wanasiasa wakifungua shule mpya zinazofundisha kwa Kiingereza katika siku za hivi karibuni! |
26 | EllyGudo jupax Steve Nicolle kipkraki amuyi kunjamatix político-nakax wali benificiado uñstapxani: | Elly Gudo alikubaliana na Steve Nicole, akidhani kwamba wanasiasa watakuwa wanufaika wakuu wa sera hii: |
27 | Nayax Steve Nicolle kipkraki amuyta. | Ninakubaliana na wewe kabisa Steve Nicolle. |
28 | Nayax Tanzania markan jakanirxamx sapxirismaw politico-nakax wali benificiado-wa tukupxani aka machaq politica-mpixa. | Kwa kuishi hapa Tanzania, ninaweza kukuambia kwa hakika kwamba wanasiasa watakuwa ndio wanufaika wakuu wa sera hii ya elimu. |
29 | Kunatix clase media ukhamarak alta ukanakax nayraru uñtasaw wal sartañ munapxi, ukat wawanakaparux kawkhantix inglés arut yatichaski uka yatichañ utanakaruw qhitapxani. | Wengi wa wa-Tanzania wa tabaka la kati na la juu ambao wanahusudu utandawazi watafanya kila wanaloweza kuwapeleka watoto wao kwenye shule zinazofundisha Kiingereza. |
30 | Ukat ukax mayninakatakix jan waliniw kunawsatix Universidad tuqiru mantañ munapkani ukhaxa ,ukampirus janiw irnaqañ jiqhatapkaspati. | Mtoto wa masikini ndiye atakayekuwa mwathirika mkuu utakapokuja wakati wa kujiunga na Chuo Kikuu na hata pale anapoanza kutafuta kazi. |
31 | Akat pä tunka maranakarux, clases sociales ukanakax payar jaljtataspäwa. | Baada ya miongo miwili, nchi [hii] itakuwa na matabaka yaliyo wazi. |
32 | Tanzania markax francés-markxama mä revolución munasi. | Tanzania inahitaji mapinduzi kama yale ya Ufaransa katika sura nyingi. |
33 | MuddybMwanaharakati jupax akham swahili arut sasi: | Akipinga sera hiyo, Muddyb Mwanaharakati alisema yafuatayo kwa Kiswahili: |
34 | Oliver Steve jan laruyistati. | Oliver Stegen usichekelee. |
35 | Jupanakax jan wali aka tuqit sapxi. | Wametia siasa ndani yake. |
36 | Wawapanakax inglés arut yatichaski uka yatiqañ utanakaruw sarapxi. | Watoto zao wanasoma international schools [shule za Kimataifa]. |
37 | Nanak pobre-nakasti sarasipkakiw jisk'a yatiqañ utanakaruxa ,ukat yatiqasipkakiw inglés arutxa iyaw, iyaw, jisa janiwa jisa janiwa sasa. | Sisi akina kajamba nani tutasoma zilezile S.t vichochoroni ili tubaki na Kiingereza chetu cha ya, ya, yes no yes no. Wakati watoto wao wanamwaga ngeli ya maana. Sijaifurahia hatua hii. |
38 | Ukampirus jumanakan wawamanakax wali suma inglés arut arst'asipxani. | Kwetu bado sana Oliver hata matangazo na sehemu nyingi ya masuala ya serikali yapo Kiingereza. |
39 | Oliver wali jayan jiqhatasisktan, kunatix gobiernunx yatiyawinakax inglés arutaskakiwa. | Josephat Rugemalira alibaini kwamba sera mpya haina mabadiliko makubwa kinyume na watu wanavyofikiri: |
40 | JosephatRugemalira sarakiwmachaq política janiw sinti jan walikiti kunjamtix jaqix amuyki ukhama: | Unahitaji kusoma kwa makini sera inavyosema: Inasema Kiswahili kitafundishwa katika ngazi zote na PIA inasema Kiingereza kitaendelea kutumika katika ngazi zote (maana yake ni pamoja na shule ya msingi). |
41 | Munasiw wali sum ullaraña kuns kamachix sasi ukxatxa: siw swahili uka arux yatichasiniw thiyapataru ukat sarakiw inglés arux yatichasiskarakiniw thiyapataruraki (akax sañ munarakiw nivel primario ukampina). Ukat nayax siristwa machaq yatiqañ utanakaw lurasispa swahili arut yatichañataki,ukhamarakiw jichhax escuelas primarias tuqinakanx inglés arut yatichasxarakispa. | Kwa hiyo tafsiri yangu ni kwamba jambo pekee jipya linalowezekana kupitia kauli kama hizi ni kuwepo kwa uwezekano kwamba sasa baadhi ya watu wanaweza kuanzisha Shule za Sekondari zinazofundisha kwa Kiswahili, na kwamba sasa ni rasmi mamlaka za serikali za mitaa zinaweza kugeuza shule za msingi zilizopo kuwa za Kiingereza. |
42 | Uka pachpa articulo tuqinpachaTrendingKenya, MargaretNjeru yatiyi kawkhantix aka machaq sistemax janiw chhaqhaykiti idioma extranjero ni payir arunaksa jan ukasti sum yatiqapxañapatakiw lurasi. | Akijibu makala hiyo hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa Trending Kenya, Margaret Njeru alieleza kwamba mfumo huo mpya wa elimu haipigi teke lugha za kigeni bali kuziweka katika nafasi sahihi katika mafunzo: |
43 | Jisnaw sum sarantañapataki. | Kwa hakika, hatua hii ni ya kijasiri na ni mwelekeo sahihi. |
44 | Yatiqawix nayrar sartañapaw ukatakix yatichasiñapaw kawknir arut yatipki uka aruta ukhamat yatiqapxañapataki. | Elimu ni maendeleo, na maendeleo yanaweza kuja tu kupitia lugha inayoeleweka vizuri kwa watu. |
45 | Uraqpachanx janiw nayrarux sartapkiti siti idioma extranjero yatichasispa ukhaxa; ukhamat idiomas coloniales uka arunakax janiw africa markarux nayrar sartañapatakix yanapkiti. | Duniani kote, hakuna nchi zinazosemekana kuwa zimeendelea zinazotumia lugha za kigeni. Matumizi ya lugha za wakoloni waliotawala nchi nyingi za Afrika yamechangia kubaguliwa kwa wananchi wengi katika mchakato wa maendeleo. |
46 | Siti nayraru sartañ munstan ukhax arusaw parlasiñapa. | Kama tunapaswa kutafsiri njia ya maendeleo ‘yetu', basi uchaguzi wa lugha lazima uende sambamba na njia hiyo. |
47 | Ukampirus akax janiw sañ munkiti idioma extranjero chhaqhayaña (payir arunaka), jan ukasti sum sarantañapatakiwa utji uka turkakipawixa. | Na hii haimaanishi kwa vyovyote kuzipiga teke lugha za kigeni (au zile tunzojifunza ukubwani), badala yake ni kuziweka katika nafasi inayozifaa katika ufundishaji na ujifunzaji. |
48 | KwameAboagyesarakiw pachaxiwa african markachirinakax arupat arsusxapxañapa: | Kwame Aboagye alisema ni wakati sasa wa-Afrika watumie lugha zao wenyewe: |
49 | Pachaxiw africa markan markachirinakax arusat arst'asxaña ,kawknirinakatix twi, yoruba, swahili ukat mandingo arunakasaxa. | Wakati umewadia nchi zetu za ki-Afrika ziongee lugha zetu wenyewe kama vile ki-Twi, ki-Yoruba, ki-Swahili na ki-Mandingo. |
50 | Nayrir pachanx inglés arux janiw jiwasan arusakiti ukat munasiw ikit sartxañasa ukhamat khitïtansa jiwasaxa yatiña. | Kiingereza hakikuwa lugha yetu ya asili na tunahitaji kuamka na kurejea misingi yetu wenyewe kwa fahari. |
51 | Aka turkakipäwix wali ch'amaniwa ukampirus nayrar sartañasawa, sarakiw Christina Higgins: | Mabadiliko hayo ni ya kihistoria lakini yanakuja na changamoto kadhaa, kama alivyobainisha Christina Higgins: |
52 | Wali suma yatiyäwiw janichä. | Habari njema kabisa. |
53 | Jichhax wali ch'amaniwa kunjamas turkakipäwix swahili arurux lurasini yänak tuqinxa, exámenes ukat yaqhanakampinakanxa. | Sasa jaribio kubwa litakuwa namna ya kutafsiri kwa Kiswahili vitabu, mitihani na zaidi. |
54 | Ukampirus turkakipäwix sinti jach'awa. | Pamoja na changamoto zake, mabadiliko haya ni ya kihistoria. |