| # | epo | swa |
|---|
| 1 | La unika nomsistemo de Birmo | Mfumo wa Kipekee wa Kuwapa watoto Majina wa Nchini Myanmar (Burma). |
| 2 | Ĉiufoje kiam birmano malkaŝas ke li aŭ ŝi ne havas familinomon, eksterlandanoj kutime demandas kial. | Pale mtu wa Burma anaposema kuwa hana jina la ukoo , wageni huwa wanashangaa ni kwa nini. |
| 3 | Birmo povas esti unu el la tre malmultaj landoj en la mondo, kie almenaŭ 90 procentoj el la loĝantaro ne havas familian nomon. | Myanmar inaweza kuwa ni miongoni mwa nchi chache duniani ambamo hadi asilimia 90 ya watu wake hawana majina ya ukoo. |
| 4 | La anoj de la sama familio povas havi tute malsamajn nomojn kaj la nombro de vortoj en ĉiu nomo povas varii grande. | Watu wa familia moja wanaweza kuwa na majina yasiyofanana kabisa na idadi ya maneno kwa kila jina inaweza kuwa na utofauti mkubwa kabisa. |
| 5 | WhatIsMyanmar skribas pri la unika nomanta praktiko en Birmo: | Mkazi mmoja wa Myanmar anaandika kuhusu utaratibu wao wa kuwapa watoto majina. |
| 6 | Sed por ni, birmanoj, familia nomo estas nur unu vorto en fabeloj skribitaj en la angla. | Anasema: Sisi wa-Myanmar, ni kama neno tu katika hadithi ziandikwazo kwa Kiingereza. |
| 7 | Kredu aŭ ne! | Amini usiamini! |
| 8 | Ni tute ne havas familian nomon. | Hatuna majina ya ukoo kabisa. |
| 9 | Kaj en ajna formularo en Birmo, estas neniu spaco por alia kesteto apud la kolumno Nomo por plenigi. | Na hakuna nafasi nyingine baada ya sehemu ya jina la kwanza katika fomu yoyote itakayotakiwa kujazwa majina hapa Myanmar. |
| 10 | Vendisto de sukerkana suko de Birmo. | Muuza juisi itokanayo na miwa kutoka Myanmar. |
| 11 | Biildo de Flickr-paĝo de Michael Foley uzita sub la CC Permesilo | Picha kutoka ukurasa wa Flirck wa Michael Foley iliyotumika chini ya mpango wa CC wa haki miliki. |
| 12 | Kaj la aŭtoro eksplikas kiel homoj el Birmo kutime plenigi formularojn, kiuj postulas kaj antaŭnomon kaj familinomon: | Na anaeleza namna ambavyo watu wa Myanmar wanavyojaza fomu zinazohitaji majina yote, yaani jina la kwanza na la ukoo: |
| 13 | Sed kiam ajn ni klopodas plenigi la retajn formularojn, ni ne havas elekton krom plenigi la spacon de familia nomo, ĉar oni markis ĝin devige. | Lakini tunapojaza fomu kutoka kwenye mtandao wa intaneti, huwa hatuna njia mbadala zaidi ya kuweka majina ya ukoo kwa kuwa ni lazima kufanya hivyo. |
| 14 | Kaj, kion ni plenigas? | Sasa, huwa tunajaza nini? |
| 15 | Por mi, mi metas du vortojn de mia nomo kiel unuan nomon, kaj la lastan vorton kiel familinomon. | Kwa upande wangu, huwa ninajaza maneno mawili ya kwanza kutoka katika jina langu kama jina la kwanza na neno la mwisho kama jina la ukoo. |
| 16 | Tre hazarda? | Unafikiri hakuna mpangilio? |
| 17 | Nu, en tiu punkto, vi eble volas scii kiom da vortoj estas en ĉiu nomo? | Vizuri, labda ungependa kufahamu kuna maneno mangapi kwa kila jina? |
| 18 | Mia saĝa respondo estas “tio dependas”. | Kwa busara kabisa, jibu langu ni kuwa “inategemea”. |
| 19 | Jes, tio tute dependas de kiel kreaj la gepatroj aŭ kiu ajn donis la nomojn estas. | Ndio, inategemea na namna wazazi walivyo wabunifu au inategemea na yule anayempatia mtoto jina. |
| 20 | Twobmad menciis kiel malfacile estas trakti birmajn nomojn en fremdaj komunumoj: | Twobmad alizitaja changamoto anazokabiliana nazo mtu pale anaposhughulikia majina ya watu wa Myanmar: |
| 21 | Mi kutime estas konfuzita, plenigante la nomon, kiel unua, meza kaj familinomo. | Huwa ninachanganyikiwa kabisa pale ninapolazimika kuandika majina yote matatu, yaani jina la kwanza, la kati na la mwisho. |
| 22 | La sama afero okazas, vivante en fremdalando, pri amikoj, kiuj ŝatus scii kiel ili vokus min. Ankaŭ ili konfuziĝas. | Hali hii pia hujitokeza pale ninapokuwa ugenini, yaani mbali na nchini mwangu, marafiki huwa wananiuliza ningependa waniite kwa jina gani. |
| 23 | Ĉar kiam ili volas voki min laŭ mia unua nomo, tio ne estas la maniero kiel mi estis vokita en mia familio aŭ en mia antaŭa komunumo. | Hakika, wao pia, huwa wanachanganyikiwa. Kwa sababu kama wakiniita kwa jina kwanza jina, sio tu kuwa hawaniiti kama nilvyokuwa naitwa katika familia yangu, lakini pia hata kwa jamii yangu iliyotangulia. |
| 24 | Ili uzas mian unuan nomon por voki min, sed mi sentas min strange se mi estas vokita per nomo, kiun mi neniam antaŭe aŭdis. | Wangeweza kuniita jina langu la kwanza, lakini ningeona kama maajabu kama ningekuwa naitwa kwa jina ambalo sikuwahi kulisikia kamwe. |
| 25 | Ba Kaung blogis pri la nompraktiko en Birmo, kiu inkluzivas ankaŭ astrologiajn kredojn: | Ba Kaung aliandika makala katika blogu kuhusiana na namna ya utoaji wa majina kwa watu wa Myanmar ambapo katika maelezo yake, alihusisha pia na imani ya elimu ya nyota: |
| 26 | Kelkaj jaroj poste, atestinte malsamajn kulturajn praktikojn tutmonde, mi rimarkis ke la birma kutimo de nomado estas sufiĉe unika. Ĝi simbolas la kombinon de la speciala virto de la persono kaj astrologia kalkulo de la tago de la semajno, en kiu la persono naskiĝis, surbaze de la luna kalendaro jaro de Birmo. | Miaka michache baadae, baada ya kushuhudia tamaduni mbalimbali duniani kote, niligundua kuwa utamaduni wa watu wa Burma wa kuwapa watoto majina ni wa kipekee kabisa kwani unajumuisha muunganiko wa kipekee wa tabia njema ya mtu huku jina likihusisha pia mahesabu ya elimu ya nyota ya mtu kwa siku ya wiki aliyozaliwa kwa kuzingatia kalenda ya mwaka itokanayo na mwezi wa wa-Barma. |
| 27 | Ĝi ankaŭ kovras la nomadon en la birma lingvo, kiu estas grava por la birma popolo sed kelkfoje konfuzas eksterlandanojn kiel “U” en “U Thant“. | Pia alizungumzia hatma ya lugha ya wa-Myanmar ambayo ni muhimu kwao na ambayo wakati mwingine imekuwa ikiwachanganya wageni, kwa mfano, “U” (inayotamkwa Oo) katika “U Thant“. |
| 28 | Krome, homoj kun unu-vortaj nomoj kutime alfrontas malfacilaĵojn difinante kial la familian nomon la unuan vorton, ekzemple “U”, “Ma”, “Daw” kaj tiel plu, kiuj ne estas iliaj nomoj teknike: | Kwa kuongezea, watu wenye majina yenye neno moja tu, mara nyingi huwa wanapata ugumu wakati wa kuelezea jina la familia, kama ilivyo kwa neno la kwanza kama “U”, Ma”, “Daw” na kadhalika, ambayo siyo majina yao kiuhalisia: |
| 29 | Esprimo de respekto estas ankaŭ unu afero de grandioza graveco por elparoli nomojn de la birma popolo. | Kuonesha heshima pia ni jambo muhimu sana katika kutaja majina ya watu wa Myanmar. |
| 30 | Oni povas esti alparolita per taŭga honoriga vorto antaŭ la donita nomo, depende de la nivelo de aĝo, laŭ parenceco, kaj laŭ sekso. | Mtu anaweza kutambulishwa kwa jina lake kutanguliwa na maneno ya heshima kwa kutegemea na umri wake, aina ya uhusiano na jinsia. |
| 31 | Diri ies nomon sen aldonaĵo estos konsiderata malĝentila alparolo. Por alparoli junulojn kaj amikojn, antaŭ iliaj nomoj: | Itachukuliwa kuwa ni jambo lisilo la heshima kumuita mtu jina kama ilivyo katika utaratibu wa kawaida wa kuongea. |
| 32 | “Ko” estas uzata kiel vira formo. “Ma” estas uzata kiel ina kaj formala formo. | Kutamka majina ya vijana na ya rika, majina yao hutanguliwa na “Ko” ambayo hutumika kutambulisha wanaume, “Ma” hutumika kutambulisha wanawake na ndio utaratibu rasmi. “ |
| 33 | “Maung” estas uzata kiel vira formala formo. | Maung” inatumika kama namna ya kuwatambulisha wanaume katika mfumo rasmi. |
| 34 | Por alparoli pliaĝulojn, antaŭ iliaj nomoj: “U” aŭ “Oo” estas uzata kiel vira kaj formala formo. | Majina ya watu wazima hutanguliwa na “U” or “Oo” ambayo hutumiwa kutambulisha wanaume katika mfumo rasmi. |
| 35 | “Daw” estas uzata kiel ina kaj formala formo. | “Daw” hutangulizwa katika majina ya wanawake katika mfumo rasmi. |
| 36 | Ĉar ne estas familia nomo por birmanoj, virinoj ne bezonas ŝanĝi ajnan parton de sia nomo eĉ post kiam ili edziĝas, Dharana skribas: | Kwa kuwa hakuna majina ya kifamilia kwa watu wa Myanmar, wanawake hawana ulazima wa kubadilisha majina yao pindi wanapoolewa. Dharana anaandika: |
| 37 | Mia tria projekto temas pri tio, kiel korekte prononci miajn kolegajn nomojn. | Mradi wangu wa tatu umekuwa ni kujifunza namna ya kutamka kwa usahihi majina ya wenzangu. |
| 38 | Birmaj nomoj dependas de tio, en kiu tago de la semajno la persono estis naskita, kaj ili ne havas unu konsistigaĵon de familia nomo. | Majina ya watu wa Myanmar hutegemea na siku ya wiki mtu aliyozaliwa na huwa hayana kipengele chochote cha majina ya kifamilia. |
| 39 | Tio signifas ke virinoj konservas sian tutan donitan nomon eĉ post geedzeco - io, pri kio miaj koleginoj ŝajnas sufiĉe fieri! | Hii inamaanisha kuwa, wanawake wataendelea kuwa na majina yao hata mara baada ya kuolewa- jambo ambalo wasichana wenzangu wananionea wivu |
| 40 | Aliflanke, kelkaj etnoj en Birmo, posteuloj de hindianoj kaj kristanoj, sekvas la praktikon havi familian nomon. | Kwa upande mwingine, baadhi ya makabila ya Myanmar, wale wenye asili ya India na wakristo wanafuata utaratibu wa kuwa na majina ya kifamilia. |
| 41 | Lionslayer skribas ke malmultaj homoj en Birmo havas familinomojn: | Lionslayer anaandika kuwa watu wachache sana wa Myanmar wana majina ya ukoo: |
| 42 | Kelkaj homoj ŝatas preni sian patran nomon, uzante britan nomsistemon. Aung San Suu Kyi estas filino de Aung San kaj Hayma Nay Win estas filino de Nay Win. | Baadhi ya watu wanapenda kutumia majina ya baba zao kwa kutumia utaratibu wa kuwapa watoto majina kwa mfumo wa Kiingereza Aung San Suu Kyi ni mtoto wa kike wa Aung San na Hayma Nay Win ni mtoto wa kike wa Nay Win. |
| 43 | Tamen vi eble malofte vidas tiujn specojn. | Hata hivyo ni nadra sana kuona utaratibu wa namna hii. |
| 44 | La birma popolo emas nomi siajn novnaskitajn bebojn laŭ astrologio anstataŭ nomi ilin laŭ iu persono. | Watu wa Burma huwa wanawapa majina watoto wao wachanga kwa kuzingatia unajimu kuliko kuwapa watoto majina kwa kuwa kuna fulani aliwahi kupewa jina hilo. |
| 45 | Kelkaj etnoj en Birmo havas familinomojn. | Baadhi ya makabila ya Myanmar kuna majina ya kifamilia. |
| 46 | Kaj kelkaj islamanoj kaj kristanoj ankaŭ nomitaj laŭ siaj patroj aŭ avoj | Na baadhi ya Waislamu na Wakristo pia huwapatia watoto majina kwa kuzingatia majina ya baba zao na babu zao. |
| 47 | Li konkludis ke la Birma registaro devus starigi familian registradon ĉar estas malfacile spuri sian familian arbon: | Alihitimisha kuwa, serikali ya Myanmar inapaswa kuweka utaratibu wa usajili kwa kuweka kumbukumbu za familia kwa kuwa ni vigumu kufuatilia chimbuko la familia ya mtu fulani: |
| 48 | Estas malavantaĝo ne havi familian nomon. | Kuna madhara ya kutokuwa na majina ya familia. |
| 49 | Estas tre malfacile spuri ies praulojn pli ol 5 generaciojn. | Ni vigumu sana kutafuta chimbuko la mtu kwa zaidi ya vizazi vitano. |
| 50 | Ne estus granda problemo, se Birmo havus familian registradan oficejon. | Sio tatizo kubwa sana kama Myanmar itakuwa na ofisi inayoratibu familia za watu wa Myanmar. |
| 51 | Mi esperas, ke la registaro starigos tian registron kaj enketan servon. | Ni matumaini yangu kuwa serikali iataweka utaratibu huu pamoja na namna nzuri ya kupata taarifa hizi. |
| 52 | Ĉiaokaze, ni ne estas solaj sur la tero sen familiaj nomoj. | Hata hivyo haijalishi kwa kuwa sio sisi tu katika ulimwengu tusio na majina ya kifamilia. |
| 53 | Mi ĵus eksciis, ke estas ankaŭ kelkaj pliaj aziaj etnoj sen familiaj nomoj. | Siku za hivi karibuni nilijifunza kuwa kuna baadhi ya makabila ya Asia ambayo pia hayana majina ya kifamilia. |