# | ind | swa |
---|
1 | Bus wisata Israel diserang di Bulgaria | Basi la Watalii Raia wa Israeli Lashambuliwa Nchini Bulgaria |
2 | Stidaknya tujuh tewas dalam serangan terhadap muda-mudi Israel yang menumpang bus wisata di Bandara Burgus di Bulgaria. | Watu wapatao saba wameuawa katika shambulio lililofanywa dhidi ya kijana raia wa Israeli katika basi lililokuwa limebeba watalii karibu na uwanja wa ndege wa Burgus nchini Bulgaria. |
3 | Menurut berbagai laporan, serangan kemungkinan dilakukan oleh pembom bunuh diri, yang mungkin berada di sisi bus maupun didalam bus. | Ripoti zinadai kuwa shambulio hilo inawezekana lilifanywa na kijana aliyekuwa amevaa bomu la kujitoa muhanga, ambaye huenda alikuwa kando ya basi ama aliingia ndani ya basi. |
4 | Menurut nrg, seorang pembom bunuh diri perempuan berdiri di depan bus dan mengkatifkan bom. | Kwa mujibu wa nrg, mwanamke huyo aliyejitoa muhanga alisimama mbele ya mojawapo ya mabasi hayo na kulilipua bomu hilo. |
5 | UPDATE: @BarakRavid: | HABARI MPYA: @BarakRavid: |
6 | Menlu Bulgaria menghubungi Menlu Lieberman dan mengatakan bahwa menurut hasil investigasi ledakan disebabkan oleh bom yang disembunyikan di bagasi bus | Waziri wa Mambo ya Nje wa Bulgaria alizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje Lieberman na kumwambia kuwa uchunguzi uligundua kwamba mlipuko huo ulisababishwa na bomu lililokuwa limefichwa kwenye buti la basi. |
7 | Perdana Menteri Israel Bibi Netanyahu mengatakan bahwa “semua petunjuk mengacu kepada Iran” dan bahwa Israel akan menjawab dengan tegas. | Waziri Mkuu wa Israeli Bibi Netanyahu alitoa tamko kwamba “dalili zote zinaelekeza kuwa Irani inahusika na mpango wa shambulio hilo” na kwamba Israeli itajibu kwa ukali. |
8 | @ruslantrad: | @ruslantrad: |
9 | bTV menunjukan foto serangan terhadap bus wisata Israel di Bulgaria | bTV ikionyesha picha za shambulio dhidi ya watalii wa Israeli huko Bulgaria |
10 | Shoshi, seorang warga Israel yang menyaksikan ledakan tersebut mengatakan: | Shoshi, raia wa Israeli aliyeshuhudia mlipuko huo alisema: |
11 | Kami melewati imigrasi dan naik ke bus #4 di luar bandara. | Tulipita uhamiaji na tukaingia kwenye basi namba 4 nje ya uwanja wa ndege. |
12 | Kami letakkan tas-tas kami, dan dua menit sesudah itu bus #2 terbakar. | Tuliweka mizigo yetu, na baada ya dakika mbili basi namba 2 liliripuka na kushika moto. |
13 | Kami dievakuasi ke dalam ruangan yang diamankan. | Kwa haraka sisi wengine tulikimbizwa kwenye chumba salama. |
14 | Puteranya menambahkan: | Mwanae wa kiume aliongezea: |
15 | Mereka yang selamat harus melompat keluar dari bus dengan berhati-hati agar tidak menginjak jenazah-jenazah. | Watu walionusurika kwenye basi iliwalazimu kuruka miili iliyotawanyika nje ya basi ili wasiikanyage. |
16 | Kami lihat bus itu, salah satu warga Israel lain memfotonya. | Tuliliona basi hilo, raia mmoja wa Israeli alipiga picha ya tukio hilo. |
17 | Kami menyaksikan bagasi bus meledak. | Tuliona buti lake likilipuka. |
18 | Kami secepatnya diungsikan ke terminal. | Tulikimbilia kwa haraka kwenye jengo la abiria. |
19 | Di laman Facebooknay, Perdana Meneteri Avigdor Liberman menulis: | Katika ukurasa wake wa Facebook, Waziri wa Mambo ya Nje Avigdor Liberman aliandika: |
20 | Saya baru saja berbicara dengan Menlu Bulgaria, Nikolay Mladenov, mengenai ledakan. | Hivi sasa nimezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Bulgaria, Nikolay Mladenov kuhusu mlipuko huo. |
21 | Mladenov sedang menuju ke lokasi dan akan memberi saya updates seketika dia tiba di sana. | Mladenov anaelekea eneo la tukio na atanipa taarifa kamili kuhusu yanayoendelea atakapofika hapo. |
22 | Siulan dari @MokedNews mengatakan: | Twiti kutoka @MokedNews inadai: |
23 | Salah satu yang tewas dalam serangan bom di Bulgaria -seorang pemandu wisata Bulgari yang berada di sana bersama para turis Israel ketika ledakan berlangsung. | Mmoja wa waliouawa katika shambulio hilo nchini Bulgaria, ni mwongozaji wa watalii wa ki-Bulgaria aliyekuwa na watalii hao raia wa Israeli mlipuko ulipotokea. |
24 | (sumber: TV Bulgaria) | (Chanzo: Televisheni ya Bulgaria) |
25 | Haaretz menayangkan liputan blog secara langsung dalam bahasa Ibrani (update anyar) dan Inggris. | Habari zaidi za moja kwa moja kwenye blogu ya Haaretz inayoandikwa kwa lugha yaki-Ebrania (habari zaidi za yanayojiri) na kwa lugha yaki-Ingereza . |
26 | Tweeps yang patut diikuti untuk update teranyar: @BarakRavid - koresponden diplomatik, surat kabar Haaretz @ruslantrad - Bloger Suriah-Bulgaria & Analis Timteng dan Maghreb @MokedNews - umpan balik berita Israel | Twiti za kufuatilia habari za moja kwa moja: @BarakRavid - Mwandishi wa kidiplomasia, gazeti la Haaretz @ruslantrad - Mwanablogu wa Syria-Bulgaria na Mchambuzi wa Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini @MokedNews - Kikusanya habari za Israeli |