# | jpn | swa |
---|
1 | グローバルなインターネットの自由を保護を求める声明 | Mradi wa Tafsiri: Kauli ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni |
2 | 11月19日から7日間かけて、グローバル・ボイスのLinguaボランティアたち[en] が、あるオンライン請願書 [en] を翻訳する。 | Katika siku saba zijazo, Wafasiri wa Kujitolea wa Mradi wa Lingua wa taasisi ya Global Voices watakuwa wakitafsiri makala maalumu ambayo ni harakati ya utetezi unaofanywa na umma mtandaoni na ambao unasaidia kulinda haki za watu kwenye mitandao ya intaneti na kuzitaka serikali zilizo wanachama wa Muungano wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu (International Telecommunication Union - ITU) kutunza matumizi huru ya Intaneti katika mkutano mkuu ujao wa ITU. |
3 | この請願書は国際電気通信連合(International Telecommunication Union, ITU)の次の会議[en] の参加者である政府の要人にインターネットのオープンさを保持するよう働きかけるものだ。 | Utetezi huu uko wazi kutiwa saini na mtu mmojammoja au asasi ya kiraia, kauli hii ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni inasomeka kama ifuatavyo: Mnamo Desemba 3, serikali mbalimbali ulimwenguni zitakutana ili kupitia upya mkataba muhimu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalojulikana kama Ushirika wa Kimataifa wa Mawasiliano ya Simu (ITU). |
4 | この「グローバルなインターネットの自由を保護する声明」は、民間組織や個人が誰でも署名できる。 内容は次のとおり。 | Kuna serikali zinazofikiri kupendekeza kupanua mamlaka ya ITU ili isimamie utawala wa Intaneti kwa njia ambazo pengine zitatishia uhuru na ubunifu katika kutumia Intaneti, huenda hatua hiyo itaongeza gharama za kutumia huduma, na hata pengine kumomonyoa haki za watu za mtandaoni. |
5 | 12月3日、世界中の政府関係者が国際連合の機関である国際電気通信連合(ITU)の条約を更新する会議に集う。 | Tunatoa wito kwa asasi za kiraia na wanaharakati wa mtandaoni kutoka mataifa yote kutia saini kwenye Kauli hii ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni: |
6 | 一部の政府はITUの権威を拡張させ、インターネットのオープンさ、革新性を脅威にさらし、アクセスにかかるコストを増大し、オンラインでの人権を侵害しうるインターネットガバナンスを提案している。 | Uamuzi kuhusu uendeshaji wa Intaneti hauna budi kufanywa kwa namna iliyo wazi kwa kuhakihisha wadau wengi mbalimbali na halisi wanashirikishwa hasa kutoka asasi za kiraia, serikali na sekta binafsi. |
7 | そこで我々はすべての国の市民社会や個人に、以下の声明に署名してもらうよう呼びかけている。 インターネットガバナンスの意思決定は市民社会や政府、民間セクターといった真正な多様な関係者の参加によって、透明性をもって行われるべきである。 | Tunaiomba ITU na nchi wanachama wake kuzingatia uwazi na kukataa mapendekezo yoyote yanayoweza kupanua mamlaka ya ITU kwenye maeneo ya uendeshaji masuala ya Intaneti yanayoweza kutishia haki za watu kwenye mitandao ya intaneti. |
8 | 我々はITUとそのメンバー国に対して、透明性を擁護するように、そしてオンラインの人権行使を脅かすインターネット統治をもたらしかねないITUの権力拡大に関するあらゆる提案を拒否するように呼びかけている。 | Ili kutia saini kwenye wito huu wa utetezi, tembelea tovuti ya Linda Uhuru wa Intaneti Ulimwenguni. |
9 | この請願書には、「グローバルなインターネットの自由を保護を求める声明」のウェブサイト[en]から署名できる。 | Ili kutia saini, andika jina lako la kwanza, la ukoo, barua-pepe yako, jina la asasi yako (ikiwa unatia saini kwa niaba ya asasi ya kiraia), weka kiungo cha URL cha asasi hiyo, na chagua nchi yako. |
10 | 署名には、名前、苗字、メールアドレス、また組織を代表しての署名の場合は組織名と組織のURLの明記、そして国名の選択が必要である。 | |
11 | カナダにあるデジタル権利の団体OpenMedia[en]の協力により、すべての翻訳は請願書のサイトでも見ることができる。 | Tafsiri zote pia zitapandishwa kwenye tovuti ya utetezi huu, ambayo imepata uhifadhi hapa OpenMedia, ambalo ni kundi la utetezi wa haki za watu la nchini Kanada. |
12 | このページの上部にも各言語での翻訳が示されているので、ぜひ友達やソーシャルネットワーク上でシェアして欲しい。 | Kadiri tafsiri zinavyojitokeza (tazama hapo juu), tafadhali washirikishe wengine pia viungo kupitia mitandao ya kijamii na marafiki! |
13 | 校正:Maiko Kamata | |