# | mlg | swa |
---|
1 | Espaina : Fanohanana Ny Tolon'ny Mpitrandraka, “Eny, Misolo Tena Anay Ry Zareo !” | Hispania: Maandamano ya Wachimbaji Madini Yaungwa Mkono na Wananchi |
2 | [rohy amin'ny teny espaniola] An'arivony ny olona nidina an-dàlam-be haneho ny firaisankina sy fanohanana ny hetsik'ireo mpitrandraka arin-tany espaniola, teo am-pahatongavana tao Madrid rehefa avy nandeha 400 km avy any avaratr'i Espaina. | Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu zaUlaya katika Migogoro. Maelfu ya watu waliingia mitaani kwa lengo la kuwaunga mkono wachimbaji wa madini wa nchini Hispania, na walijumuika nao walipowasili katika jiji la Madridi baada ya wachimba madini hao kutembea kilomita 400 wakitokea kaskazini mwa Hispania. |
3 | Ny fihetsiketsehana dia nanomboka tamin'ny 11 ora alina ny talata 10 jolay tao La Moncloa, foiben'ny governemanta, ary nifarana tao Puerta del Sol tamin'ny 2 ora maraina. | Maandamano yalianza saa 4 usiku, Jumanne ya tarehe 10 mwezi Juni katika mji wa La Moncloa, palipo na kitovu cha serikali, na yalimalizikia puerta del Sol plaza ya Madridi takribani saa 8 usiku. |
4 | Ireo mpitrandraka arin-tany dia nandà ireo fepetram-pitsitsian'ny governemantan'i Mariano Rajoya sy ny fihenan'ny fanampiana noraisiny. Ny fandraisana ny “Marcha Negra” (ny diaben'ny mainty) dia nizotra tao anaty tontolo nampihetsi-po sy sarim-piraisankina. | Wachimbaji hao wa makaa ya mawe wanaandamana kupinga mpango wa serikali ya Mariano Rajoy wa kubana matumizi pamoja na hatua ya serikali hiyo kusitisha ruzuku inayotakiwa kulipwa kwa makampuni ya uchimbaji wa makaa ya mawe ili kupunguza gharama za bidhaa hiyo kwa walaji. |
5 | Noraisina tamin'ny tehaka ireo mpitrandraka ireo, teny fankasitrahana, teny fanohanana. | Kusanyiko la kukaribisha kinachojulikana kama “matembezi meusi” (“Black March”) yalifanyika kwa ari iliyochochewa na mshikamano. |
6 | Nohirain'ireo mpanao fihetsiketsehana ireo ny hira fanevan'ny mpitrandraka, heno nandritra ny dian'izy ireo ho any an-drenivohitra. | Raia waliokusanyika hapo waliwapokea wachimbaji madini hao kwa kuwashangilia kwa kuwapigia makofi, maneno ya kuwakubali, misemo iliyoonesha kutambua hisia za wachimbaji hao wa madini pamoja na wimbo wao wa kuonesha namna wanavyo wathamini ambao uliimbwa wakati wa matembezi ya pamoja katikati ya mji mkuu. |
7 | Ireo mpitokona dia gaga tamin'ny haben'ny fanetsiketsehana izay hita ihany koa tany anatin'ny tambajotra sosialy, tamin'ny alàlan'ny fironana fantatra amin'ny anarana hoe : #nocheminera. | Wachimbaji hao walipatwa na mshangao kwa jinsi watu walivyojikusanya, jambo ambalo liliongeza chachu ya kile kinachojulikana katika mitandao ya kijamii kama #nocheminera [es] (Usiku wa uchimbaji madini). |
8 | Ny Marcha Negra tao afovoan-tanànan'i Madrid, avy amin'i Ismael Naranjo | Matembezi ya giza yakipita katikati ya jiji la Madrid. |
9 | «Eny, Azo atao !» | Picha na Ismael Naranjo. |
10 | « Eny, misolo tena anay ry zareo !» « Izao no solontenanay !», amin'ny fangalana ohatra ny fandresena vao azon'i Espaina tamin'ny Euro teo, izany no isan'ny teny faneva re nandritra ny fihetsiketsehana. | Miongoni mwa misemo maarufu ilikuwa, “Ndio tunaweza!”, “Ndio, ndio, (wachimbaji hawa) wanatuwakilisha!” na “Huu ndio mfumo wetu” wakirejelea ushindi wa hivi karibuni wa nchi ya Hispania katika kinyang'anyiro cha michuano ya mpira wa miguu barani Ulaya ambapo nchi hii ilikuwa bingwa. |
11 | Zavatra iray no mazava : ireo mpanohana ny mpiasa dia mahatsiaro mirehareha kokoa sy akaiky kokoa ny sarangan'ny mpiasa madinika noho ny mpanao politika na ny mpilalao baolina kitra. | |
12 | Nanazava ny làlan'i Madrid ireo mpitrandraka ary tsy tamin'ny jiro teny an-kandriny ihany. | Jambo moja lilikuwa wazi: wale wanaowaunga mkono wafanyakazi hawa wanajisikia fahari na wanajichanganua zaidi na daraja la wafanyakazi kuliko ilivyo kwa wanasiasa au wacheza soka. |
13 | Betsaka tamin'ireo mpanao fihetsiketsehana no manaiky tanteraka ny anton'ny fikomiana : ireo tsy manaiky lamina, ireo sorena tamin'ny hetsika 15M, ny sokajin-taona rehetra ary avy amin'ny faritra rehetra ao Espaina. | Wachimbaji wa makaa ya mawe sio tu kuwa waliangaza mitaa kwa taa walizokuwa wameziweka vichwani mwao, pia walitumia mwanga kwa waandamanaji kama ishara yenye kubeba maana pana zaidi. Sekta nyingine nyingi ziliunga mkono maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na wale wanaoipinga serikali kutoka katika maeneo mbalimbali ya Hispania. |
14 | Noho ny toe-panahim-pikomiana matanjaka miohatra amin'ny hetsi-panoherana hafa tao Espaina, ny tolon'ireo mpitrandraka dia nanjary ivon'ny fikomian'ny mpiasa madinika, sy fitsipahana an-kitsirano ny fepetra fitsitsiana ny teti-bolan'ny governemanta | Kwa kuwa yalikuwa ni maandamano yenye nia ya kuiasi serikali, zaidi kuliko maandamano mengine yaliyokwisha itishwa nchini Hispania, juhudi za wachimbaji wa madini hawa zimekuwa ni kiini cha harakati za maandamano ya wafanyakazi na yamekuwa ni hatua kali zaidi za kuipinga serikali kwa hatua zake za kutokutoa ruzuku kwa makampuni ya wachimba madini. |
15 | Ity lahatsary ity dia maneho ny hetsika firaisankina amin'ny mpitrandraka mitokona (avy amin'i Juan Luis Sánchez): | Video hapa chini inawaonesha waandamnaji wakionesha mshikamno wao pamoja na wachimba madini waliojitokeza [es] (Video na Juan Luis Sánchez): |
16 | http://youtu.be/6FeZXoupDIo | http://youtu.be/6FeZXoupDIo |
17 | Eny anaty tambajotra sosialy, maro ireo mamporisika ny mpitrandraka hanohy ny tolony manohitra ny fampihenana ny fanampian'ny governemanta izay mety hitarika fikatonan'ny sehatry ny fitrandrahana. | Kupitia mitandao ya kijamii, watu wengi waliwahamasisha wachimbaji madini kuendelea kupinga hatua ya serikali kusitisha utoaji wa ruzuku kwa makampuni ya kuchimba madini, hatua mbayo ingeweza kusababisha kufa kwa sekta ya madini nchini humo. |
18 | Ao amin'ny Twitter, maro ireo olona maneho ny hafaliany amin'ireo espaniola mpitrandraka, amin'ny alàlan'ny hafany eo ambanin'ny #yosoyminero. | Idadi kubwa ya watumiaji wa Twita walieleza kupitia twiti zao katika alama ishara #yosoyminero (Mimi ni mchambaji wa madini). |
19 | Tahaka ny hetsika teo aloha dia ny tambajotra sosialy no manaparitaka be ny vaovao, manoloana ny ambaran'ireo mpampiasa hoe #silenciomediático. | Kama ilivyokuwa kwa maandamano yaliyotangulia, mitandao ya kijamii ndiyo iliyotumika kusambaza taarifa kwa kiasi kikubwa, hatua iliyosababishwa na kile watumiaji wake walichokiita #silenciomediático (kimya cha vyombo vikuu vya habari). |
20 | Nitohy tao Madrid ny marainan'ny alarobia 11 jona ny fihetsiketsehan'ireo mpitrandraka arin-tany. | Maandamano haya ya kihistoria ya wachimbaji wa madini yalianza tena asubuhi ya Jumatano ya tarehe 11, Julai. |
21 | Na dia izany aza, nifanohitra amin'ny omalin'iny, nanamarika ny tontolo andro ny fisian'ny fifandonana teo amin'ny CRS sy ny mpanao fihetsiketsehana. | Hata hivyo, siku hii ilibadilika na kuwa ya misukosuko zaidi kuliko ile ya maandamano ya awali kutokana na waandamanaji hao kukabiliana vikali na polisi. |
22 | Niteraka naratra maherin'ny 76 sy olona am-polony voasambotra ireo fifandonana. | Zaidi ya watu 76 walijeruhiwa katika migogoro hiyo [es] na takribani watu 10 waliwekwa kizuizini. |