# | nld | swa |
---|
1 | GV Face: De strijd voor een open internet in Brazilië | GV Face: Kupigania Mtandao Huru wa Intaneti Nchini Brazil |
2 | Hecht je waarde aan de vrijheid van meningsuiting op internet? | Je, unajali uhuru wa maoni kwenye mtandao? |
3 | En aan je online privacy? | Vipi kuhusu faragha yako mtandaoni? |
4 | Hoe zou je het vinden als de regering van jouw land een wet aannam die deze rechten zou beschermen in plaats van bedreigen? | Vipi kama serikali yako ingetunga sheria ambayo ingeweza kulinda haki hizi, badala ya kuzitishia? |
5 | Braziliaanse voorvechters van digitale burgerrechten strijden al jaren voor invoering van de Marco Civil da Internet, een unieke wet die essentiële rechten en vrijheden op internet beschermt. | Watetezi wa haki za kidijitali nchini Brazili wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka mingi kupitisha Marco Civil da Internet, sheria ya aina yake inayolinda haki na uhuru mtandaoni. |
6 | De Amerikaanse digitale afluisterpraktijken hebben de kwestie nieuw elan gegeven en de steun voor het wetsvoorstel uit de hele maatschappij aangewakkerd, zelfs van de president van Brazilië, Dilma Rousseff. | Mipango ya kufuatilia mawasiliano ya watu ya Serikali ya Marekani imelifanya suala lipewe kasi mpya, likipata uungwaji mkono kutoka katika vyama vya kiraia na hata rais wa Brazil, Dilma Rousseff. |
7 | Op GV Face spreekt deze week onze editor van GV Advocacy Ellery Biddle (@ellerybiddle) met een aantal vooraanstaande deskundigen op het gebied, onder wie GV-auteur Raphael Tsavkko (@Tsavkko), Carolina Rossini (@carolinarossini) en Joana Varon (@joana_varon), die heeft meegeschreven aan het wetsvoorstel. | Wiki hii kwenye sehemu ya , Mhariri wetu wa Utetezi Ellery Biddle (@ellerybiddle) alizungumza na wataalamu waliobobea kwenye suala, mmoja wapo akiwa ni mwandishi wa GV Raphael Tsavkko @Tsavkko, Carolina Rossini (@carolinarossini) naJoana Varon (@joana_varon) mwandishi wa mwanzo wa muswada huo. Kwa viungo zaidi na maoni katika suala hili, tazama kwenye ukurasa wetu wa matukio wa Google +. |