# | pol | swa |
---|
1 | Piękne krajobrazy z Kambodży uwiecznione z drona | Picha Zilizopigwa Angani Zaonyesha Madhari Nzuri ya Cambodia |
2 | Kambodża | Sehemu ya kijijini nchini Cambodia |
3 | Podczas kręcenia dokumentu w Kambodży, reżyser Roberto Serrini [ang. ] znalazł czas, żeby odwiedzić kilka miasteczek i wsi w tym kraju. | Wakati akipiga picha za dokumentari nchini Cambodia, mtayarishaji wa filamu Roberto Serrini alipata wasaa wa kutembelea vijiji kadhaa vya mjini na vijijini katika nchi hiyo. |
4 | Jego zespół użył drona DJI Phantom i kamery GoPro, aby uwiecznić hipnotyczne piękno Kambodży. | Timu yake ilitumia ndege aina ya DJI Phantom na kamera ya GoPro kupata picha za uzuri halisi wa Cambodia. |
5 | Opisał [ang. ] filmowanie jako “wspaniałe doświadczenie”: | Alielezea zoezi hilo la upigaji picha kama ‘uzoefu wa mzuri ajabu': |
6 | Na planie w Phnom Pehn i we wsi Anluk Leak, miałem okazję odkryć piękno tego kraju z lotu ptaka. | Kwenye eneo la Phnom Pehn na kwenye kijiji cha Anluk Leak, niliweza kuchnguza uzuri wa kifilamu wa nchi hii nzuri kutoka angani. |
7 | Wspaniałe przeżycie, wiele dzieci tutaj nigdy nie widziało telewizora, nie mówiąc już o latającym dronie; mieszanka ekscytacji, obawy i zadziwienia widoczna na ich twarzach była wspaniała. | Uzoefu mzuri ajabu sana, kwa sababu wengi wa watoto hawa hawjawahi kuona televisheni, achilia mbali ndege inayopaa angani; mchanganyiko wa mvuto, msisimko na maajabu ya wanachokiona ndilo lilikuwa likionekana kwenye nyuso zao. |
8 | Poniżej zdjęcia z Flickr z podróży Roberto po Kambodży: | Hapa chini ni baadhi ya picha za kwenye mtandao wa Flickr zinazoelezea safari ya Roberto nchini Cambodia: |
9 | Krajobraz z Kambodży | Mwonekano wa kijiji kimoja wapo nchini Cambodia |
10 | Świątynia w Phnom Penh, stolicy Kambodży | Hekalu jijini Phnom Penh, mji mkuu wa Cambodia |
11 | Mnich idący przez plac | Mtawa akitembea kwenye jengo la umma nchini Cambodia |
12 | Kambodżański tuktuk, popularny środek transportu | Usafiri maarufu wa Cambodia uitwao tuktuk Hekalu jijini Phnom Penh |
13 | Świątynia w Phnom Penh Kambodżański tuktuk, trzykołowy pojazd | Pikipiki ya matairi matatu maarufu kama tuktuk ambayo ni usafiri maarufu wa umma nchini Cambodia |
14 | *Film i zdjęcia Roberto Serrini, wykorzystane za zgodą autora. | *Video na picha za Roberto Serrini, zimetumiwa kwa ruhusa yake. |