# | spa | swa |
---|
1 | Global Voices se asocia con NACLA | Global Voices Yazindua Ushirikiano na Shirika la NACLA |
2 | Global Voices y el Congreso Norteamericano sobre Latinoamérica [en] (NACLA) han puesto en marcha una nueva asociación que combina el enfoque de Global Voices en medios ciudadanos con el análisis y la experiencia de NACLA para traer a nuestros lectores la cobertura original y en profundidad sobre la región. | Global Voices na Shirika la Marekani Kaskazini Linaloshughulika na Amerika Kusini (NACLA) kwa pamoja wameanzisha ushirikiano ambao utaunganisha dira ya ‘Sauti za Dunia' ya uanahabari wa kiraia pamoja na ile ya NACLA ya uchambuzi na utoaji wa elimu, lengo likiwa ni kuwaletea wasomaji wetu habari halisi na za kina kutoka katika eneo hili la Latini Amerika. |
3 | NACLA [en], fundada en 1966, es una organización independiente, sin fines de lucro que busca “fomentar el conocimiento más allá de las fronteras”, proporcionando información y análisis sobre América Latina y su compleja relación con los Estados Unidos | NACLA, lililoanzishwa mwaka 1966, ni shirika huru, lisilo la kimaslahi lililo na lengo la “kuendeleza maarifa bila mipaka” kwa njia ya kutoa taarifa na uchambuzi kuhusu Latini Amerika pamoja na hali tete ya ushirikiano kati yake na Marekani: |
4 | “Creemos que el conocimiento es esencial para el cambio, así que utilizamos una combinación única de información / activismo de los medios y educación popular para proporcionar a las personas las herramientas que necesitan para comprender el mundo para así cambiarlo” | “tunaamini kuwa maarifa ni muhimu sana katika mabadiliko, kwa hiyo, tunatumia muunganiko wa kipekee kabisa wa taarifa/uanaharakati wa vyombo vya habari na elimu ya kawaida ili kuwapatia watu vitu wanavyovihitaji ili kuweza kuuelewa vizuri ulimwengu na kisha kuwa na uwezo wa kuubadili” |
5 | Cada mes, autores de GV y NACLA trabajarán juntos para proporcionar contenido relacionado con un tema específico. | Kila mwezi, waandishi wa GV(Sauti za Dunia) na NACLA watakuwa wanafanya kazi kwa pamoja ili kutoa habari zitakazokuwa zinazungumzia mada moja. |
6 | Un podcast con entrevistas, análisis e información adicional sobre los temas analizados en las publicaciones estará disponible a finales de mes. | Podikasti yenye mahojiano, uchambuzi na taarifa za ziada kuhusiana na mambo yaliyojadiliwa kwenye makala mbalimbali zitapatikana kila mwisho wa mwezi. |
7 | Travesías de inmigrantes | Safari za Wahamiaji |
8 | Comenzamos nuestra colaboración con el tema “Travesías de inmigrantes”. | Tunaanza ushirikiano wetu kwa kuanza na mada ya “Safari za Wahamiaji”. |
9 | En julio estaremos cubriendo una amplia gama de temas relacionados con la migración: Desde el Proyecto de ley de inmigración que se está debatiendo actualmente en el Congreso de Estados Unidos, a las historias humanas detrás de los migrantes que realizan peligrosas travesías al norte a través de América central y México. | Mwezi Julai tutakua tukizungumzia kwa mapana kabisa mambo yanayohusiana na uhamiaji: kutoka kwenye Mswada wa Uhamiaji ambao kwa sasa unajadiliwa katika bunge la Marekani, hadi kwenye habari kuhusu safari ngumu na ndefu za wahamiaji kutoka Kaskazini mwa Amerika kupitia Amerika ya Kati hadi nchini Mexico. |