# | srp | swa |
---|
1 | Arapski svet: “Prestanite da plačete nad Sudanom” | Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani” |
2 | Današnji referendum o nezavisnosti stavio je Sudan na radar arapske tviterosfere. | Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. |
3 | Od Saudjske Arabije do Palestine, arapski tviteri diskutuju jedinstvo Sudana, podelu i [njegove] resurse. | Kuanzia Saudia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani. |
4 | Ovaj referendum je deo sporazuma iz 2005. između Khartoum central governmenti i Narodno oslobodilaćke vojske Sudana i mogao bi značiti odvajanje južnog Sudana od ostatka države. | Kura hii ya maoni ni sehemu ya Makubaliano ya Naivasha yaliyofanyika mwaka 2005 baina ya serikali kuu ya Khartoum na Chama cha SPLA (Sudan People's Liberation Army) na inaweza kusababisha kumeguka kwa Sudani ya Kusini kutoka kwenye nchi ya Sudani ya leo. |
5 | Omar Alattas iz Saudijske Arabije pita: | Kutoka Saudi Arabia, Omar ALattas anauliza: |
6 | Kada će biti objavljeni rezultati referenduma? | Matokeo ya kura ya maoni ya Sudani yatatangazwa lini? |
7 | I potom zaključuje: | Na anahitimisha: |
8 | Danas će, kao najveću arapsku zemlju, Alžir zameniti Sudan. | Leo nchi ya Aljeria itachukua nafasi ya Sudani kama nchi kubwa zaidi ya Kiarabu |
9 | Bader Aujan, takođe iz Saudijske Arabije, pozitivno gleda na budućnost: | Bader Aujan, kutoka Saudi Arabia pia, ana mtazamo chanya kuhusu mustakabali (wa Sudani): |
10 | Nemačka se ujedinila posle podele;Hong Kong se vratio Kini posle odvajanja; I ja se nadam da će se Sudan vratiti. | Ujerumani iliungana tena baada ya kugawanyika; Hong Kong ilirudi China baada ya kujitenga; na ninategemea vilevile kwamba Sudani itakuwa hivyo hivyo. |
11 | Nadam se da će ovo odvajanje biti snažan podstrek za razvoj. | Ninatumaini utengano huu utakuwa kichocheo muhimu kwa ajili ya maendeleo. |
12 | On dalje dodaje: | Halafu anaongeza: |
13 | Nemačka je odličan primer kako se podeljene zemlje jednog dana mogu ponovo mirno ujediniti. | Ujerumani ni mfano mzuri wa namna nchi zilizowahi kujitenga siku moja zilikuja kuungana tena kwa amani. |
14 | #Sudan nije izuzetak! | #Sudan haiwezi kuwa tofauti katika hili! |
15 | Mohamed Osman, koji takođe tvituje iz Saudijske Arabije, apeluje na svoje čitaoce: | Na Mohamed Osman, ambaye pia anatuma habari kwa njia ya Twita kutoka Saudi Arabia,, anawasihi wasomaji wake: |
16 | Draga arapska braćo, molim vas prestanite da plačete i pravite problem od Sudana. | Wapendwa ndugu zangu wa Kiarabu, tafadhali acheni kulia na kutengeneza mizengwe kwa yanayotokea Sudani. |
17 | Imali ste dvadesetšestogodišnji rat u kome ste bili mirni. | Kulikuwa na mapigano ya miaka 26 ambapo ninyi mlinyamaza. |
18 | Molim vas, nastavite da ćutite. | Tafadhali endelezeni kimya chenu leo. |
19 | Palestinac Bahaa AlKayyali se moli za ujedinjeni Sudan: | Mpalestina Bahaa AlKayyali anaombea umoja wa Sudani |
20 | Jedinstvo za Sudan, jedinstvo. | Umoja kwa Sudani…umoja |
21 | Dok Ali Dahmash iz Jordana ukazuje na bogate resurse Sudana: | Wakati kutoka Jordani, Ali Dahmash anaonesha Rasilimali zenye utajiri za Sudani: |
22 | Da li znate da je 70% sudanske proizvodnje nafte locirano na jugu? | Hivi mnafahamu kwamba asilimia 70 ya uzalishaji wa Mafuta ya Sudani yako kusini? |
23 | Nije čudo zašto John Kerry i američki političari podržavaju podelu! | Si ajabu John Kerry & wanasiasa wa Kimarekani wanaunga mkono utengano! |
24 | Vraćamo se u Saudijsku Arabiju, gde se Bandar Bin Naif pita: | Na huko huko Saudi Arabia, Bandar Bin Naif, anajiuliza: |
25 | Jedan satelit je specijalno lansiran za praćenje referenduma u Sudanu. | Chombo cha kurekodi mawasiliano angani (Setilaiti) kilirushwa mahususi kwa ajili ya kufuatilia kura ya maoni na maendeleo ya nchi ya Sudani. |
26 | Da li se ovo radi zbog ljubavi prema Sudanu ili kao blagoslov za ofvajanje? | Je, hili linafanyika kwa kuipenda Sudani ama ni baraka kwa ajili ya kujitenga |