# | swa | swe |
---|
1 | Uchafuzi wa Hewa wa Kutisha Jijini Tehran Waanikwa | Tehrans dödliga luftföroreningar i bild |
2 | Uchafuzi wa hewa umekuwa adui wa umma kwa mamilioni ya watu wa Tehran kwa miaka mingi sasa. | Luftföroreningar har varit allmänhetens fiende för miljontals iranier under flera år. |
3 | Hivi leo, si habari za kushangaza tena kusikia kuwa siku fulani serikali imesitisha huduma katika taasisi za serikali kwa sababu ya uchafuzi wa hewa. | Det kommer inte längre som en nyhet när myndigheterna vissa dagar stänger ner offentliga institutioner p.g.a. luftföroreningar. |
4 | Mapema mwezi huu, Wizara ya Afya, ilitangaza kuwa katika mwaka uliopita zaidi ya watu 4, 400 walipoteza maisha kutokana na uchafuzi wa hewa huko Tehran, mji mkuu wa Iran. | Tidigare denna månad deklarerade hälsoministeriet att 4 400 människor dog under förra året till följd av luftföroreningar i Tehran, Irans huvudstad. |
5 | Tehran iliyofunikwa Vumbi | Dammiga Tehran |
6 | Kuna baadhi ya katuni zinazosambazwa na watumiaji wa mtandao wa nchini Iran kuhusiana na uchafuzi huo wa hewa mjini Tehran. | Ett flertal skämtteckningar har delats bland iranska nätanvändare om Tehrans föroreningar. |
7 | Omid alichora katuni katika mtandao wa Iroon.com ili kuonesha Tehran ilivyofunikwa na vumbi. | Omid har ritat en karikatyr på Iroon.com som visar hur dammigt Tehran är. |
8 | Omid, Iroon.com | Omid, Iroon.com |
9 | Mana Neyastani hakuacha kupiga siasa kwa kutumia katuni kuhusiana na uchafuzi huu: “Babu” anasema “Kumekucha tena, na ninapaswa kuamka… habari mbaya hizi…adhabu, jela…” “Babu” anavuta pumzi nzito ili kuianza siku yake na kuanguka chini kando ya jarida lenye kichwa cha habari: “Uchafuzi uliokithiri wa hewa ya Tehran” | Mana Neyastani glömde inte bort politiken i sin tecknade serie om föroreningar: “Farfar” säger “Det är morgon igen, och jag borde stiga upp… alla dessa dåliga nyheter… avrättningar, fängelsestraff…” Farfar” tar ett djupt andetag för att börja sin dag och faller död ner bredvid en tidning med rubriken: “Dödlig luftförorening i Tehran” |
10 | Mana Neyestani, Mardomak. | Mana Neyestani, Mardomak. |
11 | Jiji la Giza | Mörk stad |
12 | Ifuatayo ni video inayoonesha Tehran iliyochafuka kwa moshi mweusi wakati wa adhuhuri, muda ambao ndege ilikuwa inatua katika uwanja wa ndege wa Mehrabad. | Här är ett videoklipp som visar ett flygplan som landar på Mehrabads flygplats i ett mörkt förorenat Tehran vid lunchtid. |
13 | Hakuna Hewa ya Oksigeni | Inget syre |
14 | Mwanablogu wa Iran ajulikanaye kwa jina la Zeyton, anasema [fa]: | Zeyton, en iransk bloggare, säger [fa]: |
15 | Tulizoea kusema kuwa hakuna sehemu ya kupumulia katika nchi hii. | Förr sade vi att det inte finns plats att andas i det här landet. |
16 | Kwa kusema hivi, tulikuwa na maana ya ukandamizaji wa kisiasa na wa kijamii uliofanywa na serikali. | Med det menade vi att det rådde politiskt och socialt förtryck av regimen. |
17 | Lakini kwa sasa, kiuhalisia hakuna hewa ya Oxygen ya kuvuta. | Men nu finns det bokstavligen inget syre att andas. |
18 | Serikali isiyoweza kuhakikisha watu wake wanapata hewa ya Oxygen ya kutosha ndiyo hii inayojigamba kuonesha mfano wa kuigwa wa kiutawala ulimwenguni kote. | En regim som inte kan ge sina medborgare syre att andas säger sig vilja exportera sitt sätt att styra landet till hela världen. |
19 | Tusisahau kuwa watu katika miji mingine mingi nchini Iran nao pia wameshakuwa wahanga wa uchafuzi huu, kama ilivyo kwa jiji la Kaskazini,Ahwaz [fa]. | Vi ska inte glömma att människor i andra städer i Iran också har fallit offer för föroreningar, som t.ex. staden Ahwaz [fa] i södra Iran. |