# | swa | urd |
---|
1 | Morocco: Wanafunzi Wadai Marekebisho kwenye Mfumo wa Elimu | مراکش ۔ طالبِ علموں کا فرسودہ تعلیمی نظام کو تبدیل کرنے کا مطالبہ۔ |
2 | Mwezi Julai, kundi la wanafunzi wa Morocco lilizindua ukurasa wa Facebook uitwao “Muungano wa Wanafunzi wa Morocco kubadili mfumo wa Elimu” (ufupi kwa Kifaransa: UECSE). | جولائی میں مراکش کے طالبِعلموں کے ایک گروپ نے سماجی رابطے کی ویب سائٹ فیس بْک پر ایک پیج شروع کیا جس کا نام Union of Moroccan Students to Change the Education System (فرانسیسی مخفف UECSE)ہے۔ |
3 | Kundi hilo ni mkusanyiko wa vijana wa Morocco ambapo lengo lao ni “kuchukua hatua, na kujadili ufumbuzi madhubuti wa kukuza ubora wa mfumo wa elimu”. | اِس گروپ کا مقصد مراکش کے تعلیمی نظام کو بہتر بنانے کی حکمتِ عملی تیار کرنا ہے۔ |
4 | Ndani ya muda usiotimia mwezi mmoja tayari ukurasa huo uliwavutia wanachama zaidi ya 10,000 na kupata uungwaji mkono kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii. | ایک مہینے کے اندر اِس پیج پر 10,000 افراد نے اِس مہم میں اپنا ساتھ دینے کا اِظہار کیا ہے۔ |
5 | Yaonekana jambo zima lilipata kasi zaidi kufuatia taarifa kwamba serikali ilikuwa na mipango ya kushupaza sera ya masomo katika vyuo vikuu vya umma. | میڈیا کا کہنا ہے کہ اِس مہم کو شروع کرنے کی وجہ ، سرکاری یونیورسٹیوں میں ٹیوشن پالیسی کی سختی ہے۔ |
6 | Kikundi kiliitisha [Fr] maandamano ya nchi nzima mnano Jumapili Agosti 6, 2012, na “kuhamasisha asasi za kiraia na wasomi wanasiasa wa Morocco kuanzisha mjadala wa kitaifa juu ya hatua za kurekebisha mfumo.” | 6 اگست 2012 کو اِسی سلسلے کے تحت ایک ملک گیر اِحتجاج کا اِنعقاد کیا گیا جس میں عوام الناس اور سیاسی شخصیات کو دعوت دی گئی تا کہ وہ مراکش کے تعلیمی نظام کو بہتر بنانے کے لئے اپنی رائے دے سکیں۔ |
7 | Wito huo ulisambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. | سوشل میڈیا نے اِس مہم میں اِہم کردار ادا کیا۔ |
8 | Kupitia video ambayo kundi hilo liliituma kwenye YouTube kabla ya maandamano kufanyika, wanafunzi walitoa wito wa kufanyika mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu. “Mfumo mzima wa elimu unahitaji kubadilishwa,” mwanafunzi mmoja anasema mbele ya kamera. | احتجاج سے قبل یو ٹیوب پر ایک ویڈیو نشر کی گئی جس میں مختلف خیالات کا اِظہار کرتے ہوئے طلباء نے کہا ''تعلیمی نظام کو مکمل طور پر نئے سرے سے شروع کیا جانا چاہیئے۔ |
9 | “Mfumo unahitaji kuvunjwa kabisa na kuundwa upya kutoka mwanzo,” anasema mwingine. | ‘‘ ایک اور طالبِ علم کا کہنا تھا کہ ''موجودہ تعلیمی نظام کو ختم کر دینا چاہیئے ۔‘‘ |
10 | Wengi wa wanafunzi wanaoonekana kwenye video pia wamekemea kile wanachokiona kuwa “hatua zisizomotisha” zilizowekwa juu mno na Grandes Ecoles, hasa katika viwango vya kushindaniwa kupitia mitihani ya kujiunga na chuo. | بہت سے طلباء کا یہ کہنا تھا کے Grand Ecoles کے تحت اِمتیازی نمبروں سے پاس ہونے پر کالجوں اور یونیورسٹیوں میں داخلہ ملنا باقی طلباء و طالبات کے لیے نا انصافی ہے۔ |
11 | Katika siku ya maandamano, mamia ya wanafunzi na wazazi wao waliitikia mwito wa kuandamana kama inavyoonyeshwa kupitia picha na video zilizochukuliwa na kisha kuwekwa mtandaoni. | اِحتجاج کے روز نہ صرف طلباء بلکہ اْن کے والدین نے بھی انٹرنیٹ پر کی جانے والی اپیل کی بھرپور حمایت کی۔ |
12 | Picha ya video ifuatayo ni kutoka katika maandamano yaliyofanyika katika jiji kubwa zaidi la nchini Morocco, Casablanca (zilizowekwa na The7Gladiator): | درجِ ذیل ویڈیو مراکش کے سب سے بڑے شہر کاسا بلانکا میں ہونے والے اِحتجاج کا ایک منظر پیش کر رہی ہے۔ |
13 | Picha zilizowekwa kwenye mtandao wa Flickr na Hassan Ouazzani zinaonyesha utofauti mkubwa wa itikadi za kukemea rushwa, upendeleo, miundombinu duni na masharti magumu yanayowekwa dhidi ya wahitimu wa shahada ya kwanza wanaotaka kuendelea na elimu ya juu zaidi: | پر حسن اوزانی کی نشر کی ہوئی کچھ تصاویرجو کے مراکش کے تعلیمی نظام میں موجودہ مسائل جیسے بے ترتیب نظام ، رشوت ، اور یونیورسیٹیوں میں داخلے کی سخت پالیسیوں کی عکاسی کرتی ہیں۔ |
14 | Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu - Picha kwa niaba ya Hassan Qazzani - Imetumiwa kwa ruhusa | مراکش کے طالبِ علموں کاموجودہ تعلیمی نظام کے خلاف اِحتجاج۔ تصویر حسن اوزانی |
15 | Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu - Picha imetumiwa kwa idhini kutoka kwa Hassan Quazzani | اِحتجاج کے تمام مراحل پْر امن رہ کر طے کیے گئے۔ |
16 | Wanafunzi wa Morocco watoa wito kwa ajili ya mageuzi ya mfumo wa elimu - Picha imetumiwa kwa idhini kutoka kwa Hassan Quazzani | اِس گروپ نے پورے مْلک میں مزید اِحتجاجی مظاہرے اِنعقاد کروانے کا فیصلہ کیا ہے۔ |
17 | Maandamano yaliendelea kwa amani. | :کا کہنا ہے کہ UECSE پرTumblr |
18 | Kundi hili liliahidi kuandaa migomo ya chini kwa chini na mikutano zaidi nchini kote. Kwenye Tumblr, UECSE iliandika: | نوجوان طالبِ علم ایک بہتر تعلیمی نظام چاہتے ہیں۔ |
19 | WANAFUNZI vijana wanaomba kuwepo kwa mfumo bora zaidi wa elimu kwa ajili yao wao kama WANAFUNZI WA MOROCCO, kwa kuwa wamechoshwa na hali ya sasa wana nia ya kubadili hali zao za baadaye (e) ili kutimiza ndoto za maishani mwao, wimbi lenye mshawasha motomoto lajionyesha wazi. | یہ مراکش کے وہ طالبِ علم ہیں جو کہ موجودہ نظام کو بدل کر اپنا مستقبل روشن اور تابناک بنانا چاہتے ہیں۔ اس مہم کے ذریعے تعلیمی نظام میں تبدیلی کی اْمید کی کرن نظر آ رہی ہے۔ |