# | swa | zhs |
---|
1 | Kambodia: Je, Viwango vya Maadili Miongoni Mwa Watawa Vinaporomoka? | 柬埔寨:和尚越来越没品? |
2 | Kwa kuwa dini ya Kibuda ni dini ya dola kwa mujibuwa Katiba ya nchi ya Kambodia, hasa kwa kuzingatia kwamba karibu raia wote wa Kambodia ni Wabuda, matukio yaliyoripotiwa hivi karibuni kuhusu kuporomoka kwa maadili nchini humo miongoni mwa watawa ni jambo la kutilia maanani. | 由於佛教是柬埔寨宪法中注明的国教,几乎所有的柬埔寨国民都是佛教徒,因此最近报导中传出国内和尚的德性越来越差这件事引起关注。 |
3 | Watawa wameripotiwa kushiriki katika matukio kadhaa yaliyohusisha utumiaji nguvu au utovu wa nidhamu ikiwemo kushiriki tendo la ngono au kutazama picha na video za ngono. | 在许多场合中,有人发现和尚从事暴力行径,或是与他人性交、看色情刊物等等不当行为。 |
4 | Kuna kisakilichomhusisha mtawa kiongozi aliyeripotiwa kulewa na kisha kumpiga mwanakleri (mtawa) mwingine huku mwanakleri huyo akishindwa kulipigia jambo hilo ripoti kwa sababu za kiusalama,hasa kwa kuwa mtawa kiongozi huyo anafahamika vema kwamba yeye ni kama mtawa mfalme katika jimbo linalohusika. | 有个案例是关於一位省级住持喝醉了,打伤了一名僧侣,然而他为了保护自己的安全,没有报案。 |
5 | Hivi karibuni , kuna mtawa aliyekamatwa akichukua picha za video za wanawake waliokuwa uchi ambao walikuwa wamekwenda kwenye monasteri ili kujichotea maji yanayoaminika kuwa ya baraka, ambapo inaaminika kwamba maji yanayotolewa na mtawa huyo huwaondolea watu bahati mbaya na kuwafutia mambo yote mabaya. | 只因这位住持位居该省和尚中最高层级,是为国王和尚。 |
6 | Upelelezi uliosababisha kukamatwa kwa mtawa huyo ulitokana na kusambazwa kwa picha hiyo ya utupu ya video kwa watu wengi hasa kupitia zana za bluetooth za kwenye simu za mkononi. | 最近,有名和尚因为制作裸体女性的影片而被抓,这些女性是为了求妙水而来,据说那位和尚给的水可以辟除各种坏事并带来福份。 |
7 | Jambo hili nalo kwa upande mwingine liliibua swali kubwa kuhusu muundombinu wa teknolojia ya kisasa na maendeleo yake nchini Kambodia ambapo sasa hivi watu wanaweza kujipatia picha za utupu kwa urahisi zaidi. | 之所以展开调查并逮捕和尚是因为发现大量的裸体影片透过蓝芽手机交换而追踪到的。 这显然引发对於柬埔寨科技基础建设逐渐发展的质疑,因为人人都可以更简单地接触色情内容。 |
8 | Hata hivyo, kama ilivyopendekezwa na Chan Nim, masuala ya namna hii yanaachwa kwa mtu mwenyewe na dhamiri yake hasa kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia hizi zinazoibuka. | 然而,正如Chan Nim 所说,这个议题由科技使用者的良心来决定。 |
9 | Kwa upande mwingine, wapo watawa wengi tu ambao wanaelewa nafasi ya teknolojia katika kuhamasisha mafundisho ya kidini. | 另一方面,有许多操守高洁的和尚了解科技在推广宗教教诲上的角色。 |
10 | Wakati ambapo hivi sasa ni jambo la kawaida kuona blogu nyingi zinazoanzishwa na vijana wanaojadili masuala ya kijamii, ya kiteknolojia au ya kibinafsi, sasa kuna hata pia blogu zenye kubeba ujumbe wa Imani ya Buda kama vile Bodhikaram, Saloeurm, Khmerbuddhism. | 现在可以普遍见到许多年轻人开设的部落格,上头讨论社会、科技、或个人议题,同时也有佛教主题的部落格,像是Bodhikaram, Saloeurm, Khmerbuddhism 等等。 |
11 | AMafundisho ya kina ya falsafa ya Ki-Buda hivi sasa yanapatikana kwenye mtandao wa Intaneti katika muundo wa maoni mafupimafupi, kamusi, podikasti, na hata vitabu kamili ivilivyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza na Khmer. | 广泛的佛教哲学教诲现在可以在网路上透过各种形式供人近用,像是佛家短语、佛教字典、播客、或是经书等等,有高棉语跟英语。 |
12 | Zaidi ya hilo, kuna idadi kubwa tu ya watawa ambao wanatumia Intaneti kwa wingi zaidi ili kujaribu kuwafikia watu wengi zaidi. | 除此之外,有许多和尚透过网路加强传教,接触更广大的阅听人。 |
13 | Kwa mfano, Mtukufu Saloeurm Savath, amekuwa akifanya juhudi kubwa kueneza mafundisho ya KiBuda kupitia ukurasa wa face-book ambao sasa umekuwa kama uwanja muruwa unaomwezesha yeye na wafuasi wake kuwasiliana naye kwa urahisi na hasa pale wanapohitaji maelezo zaidi kuhusu Kanuni za KiBuda au masuala mengine. MaPagoda na watawa ni sehemu muhimu ya urithi wa kiutamaduni na elimu ya Wakambodia. | 例如可敬的Saloeurm Savath 就严格地在脸书(facebook)上分享诸多佛教教诲,与他的信徒自然地联系,信徒也可以透过脸书向他请教佛教宗旨或议题。 |
14 | Wanaendelea kutoa mchango mkubwa kwa jamii nzima. Ni matumaini kwamba masuala ya maadili ya watawa yatazingatiwa zaidi ili kuwahimiza watu kujiimarisha zaidi katika imani yao na kuamini kwao imani ya KiBuda. | 佛塔跟和尚是柬埔寨文化跟教育珍贵遗产,持续贡献社会。 |
15 | Imani hiyo imechangia sana katika upatanisho wa kitaifa na amani ya kisaikolojia, hasa katika suala la watu walionusurika kufa mikononi mwa Utawala wa Khmer Rouge. | 大家期待和尚的德性可以加强,好让人们能自我肯定对佛教的信仰跟信心,更何况佛教对於国内和解跟精神平和有过很大的贡献。 |
16 | Watu hawa waliendelea kufuata mafundisho ya KiBuda na hasa katika kujirekebisha mwenendo wao ili kufutilia mbali shauku yao ya kulipiza kisasi na kutawala hasira zao na badala yake kuwa na matumaini na mtazamo wa kutafuta amani zaidi. | 例如赤柬政权时代的幸存者就持续透过佛家教诲,将他们内心的报复心跟愤怒心转换成希望跟平和。 |