# | swa | zht |
---|
1 | Pasipoti za Kidiplomasia kwa Viongozi wa Kidini nchini Brazil? | 巴西:宗教神職代表可持有外交護照? |
2 | Hivi karibuni mjadala mkali umepamba moto nchini Brazil baada ya Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa, inayoitwa Itamaraty, kutoa pasipoti mbili za kidiplomasia [pt] kwa viongozi wa makanisa ya kiinjili Igreja Mundial do Poder de Deus (Kanisa la Dunia la Nguvu la Mungu/World Church of the Power of God) mchungaji Valdemiro Santiago de Oliveira na mke wake Franciléia de Castro Gomes de Oliveira. | 最近巴西正在熱烈討論一起爭議事件,風波始於該國外交部,別名又稱Itamaraty,簽發兩本外交護照給「上帝權能世界教會(World Church of the Power of God)」的牧師長Valdemiro Santiago de Oliveira和他的妻子Franciléia de Castro Gomes de Oliveira。 |
3 | Nchini Brazil utoaji wa pasipoti za kidiplomasia unadhibitiwa na katiba ya nchi Kifungu ya 5.978 [pt] kinachotamka kuwa nyaraka hizo rasmi zinaweza kutolewa kwa marais, makamu wa rais, mawaziri, wabunge, wakuu wa idara za kidiplomasia, majaji wa mahakama kuu na marais waliopita. | 依據巴西憲法法令第5. 978條之內容,外交護照的持有特許權受到管制,這些官方文件只能簽發給總統、副總統、部會首長、國會議員、使館使節、最高法院院長、與卸任元首。 |
4 | Hata hivyo, pasipoti za kidiplomasia zimekuwa zikitolewa kwa wawakilishi wa Kanisa Katoliki, kwa kutumia tafsiri ya Ibara ya 6, kifungu cha 3: | 但是根據巴西憲法第五條第三段內容之解釋文,外交護照依照慣例也能簽發給天主教會的神職代表。 |
5 | Picha ya Mchungaji Valdemiro Santiago iliyotoka kwenye ukurasa wake wa wazi wa Facebook | 此照片為Valdemiro Santiago牧師,取自本人公開的臉書頁面。 |
6 | …kwa watu ambao, ingawa hawajaorodheshwa katika ibara hii, wanahitaji kuipata ili kutimiza majukumu yenye maslahi ya nchi. | …如對本國整體利益具有重要影響者,雖不符本條文中各項身份描述,仍可予以簽發外交護照。 |
7 | Ingawa, kama ilivyotajwa awali, Makadinali wa Kanisa Katoliki wamekuwa wakinufaika na takwa hilo la kikatiba, taasisi nyingine za kidini zinazotambuliwa na serikali ya Brazil hazijatengwa katika kuomba pasipoti za kidiplomasia na hata wakuu wengine wa madhehebu ya kiprotestanti, kama mchungaji ambaye ni vigumu kueleweka kirahisi Edir Macêdo, kiongozi wa Kanisa la Ulimwengu (Igreja Universal) walipokea pasipoti za kidiplomasia siku za nyuma. | 如以上文字所述,儘管天主教會的樞機主教擁有這項特許權,不過其它獲得巴西政府承認的宗教團體同樣也能申請外交護照,像是新教傳教士在過去也持有過外交護照,如備受爭議的巴西普世 (Universal Church)教會牧師長Edir Macêdo。 |
8 | Tushukuru siku hizi kuna uwazi ulioletwa na vyombo vya habari ambao uliwezesha jambo hili kufahamika na kufikia Wizara husika kupata upinzani mkali kutoka kwa raia watumiao mtandao kufuatia uamuzi huo. | 由於媒體對此單一事件的渲染,巴西外交部因此飽受網友嚴厲抨擊,並引起一連串針對宗教團體權力與違背憲法政教分離精神的討論。 |
9 | Ukosoaji wa hatua hiyo umechochea kwa namna mpya mjadala uliokuwepo wa mamlaka ya taasisi husika na kukiukwa kwa dhana ya nchi kutokuwa na dini kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo. | 巴西Folha de São Paulo報的讀者Renato Khair對此事件的報導發表以下看法: |
10 | Msomaji wa gazeti la Folha de São Paulo, Renato Khair, alituma maoni yafuatayo akijibu makala [pt] iliyokuwa ikiangazia suala hilo: Ni jambo lisilokubalikaa kwa serikali kuitumia Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa kutoa pasipoti za kidiplomasia kwa Kanisa liitwalo World Church. | 我無法接受政府放縱外交部,將外交護照的特許權開放給「世界教會」,這是錯誤的作法,例如巴西前總統魯拉(Lula)之子、受到質疑的教會牧師,以及其他許多人都未合法持有外交護照,外交部這種作為讓其它優秀且嚴謹的政府單位一同蒙羞。 |
11 | Ni kupotoka kuona watu wasiokidhi vigezo vya kisheria wanapokea pasipoti za kidiplomasia, kama watoto wa Rais wa zamani Lula, Makasisi watajwa na wengine wengine. | 部落客Parsifal Pontes也對此次外交護照的簽發事件提出批評並強調一點: |
12 | Kinachofanywa na Wizara ya Mahusiano ya Kimataifa ni kudhalilisha taasisi ambazo awali zilionekana kama zenye heshima na zenye umakini katika utendaji wake. | 我國外交部不把外交護照的特許權當做一回事,遲早一本又一本的外交護照會讓各國海關貽笑大方。 |
13 | Mwanablogu Parsifal Pontes vilevile alikosoa [pt] utoaji huo wa pasipoti za kidiplomasia kwa kusisitiza: | 上帝權能世界教會。 |
14 | Namna tu wizara yetu inavyochukulia kiwepesi suala la kutoa pasipoti za kidiplomasia na kutumia vibaya mamlaka yake itasababisha idara za uhamiaji nje ya nchi waangue vicheko wanapoona aina ya watu wanaotembea na nyaraka hizo. | 圖片來源:Roberto Castelhano的Flickr 。 |
15 | Igreja Mundial do Poder de Deus. Picha ya Roberto Castelhano kwenye mtandao wa Flickr. | 依據創用CC BY-NC-ND授權使用。 |
16 | (CC BY-NC-ND 2.0). Kwenye Mtandao wa twita, kupitia alama habari #estadolaicoja (nchi isiyo na dini sasa) mwenendo wa majadiliano unaonyesha kuwa nchi ya Brazili imevuka mipaka kwa kuvunja kanuni za msingi za nchi kutokufungamana na dini dhana ambayo ilipaswa kuheshimiwa. | estadolaicoja(現代世俗國家)在推特上寫到,一般輿論都認為巴西政府表現太過離譜,竟然違背大眾期待的政教分離原則。 |
17 | Lawyer Thiago G. | 律師Thiago G. |
18 | Viana (@thiago_fiago), ambaye hublogu na Comendo o Fruto Proibido, alitwiti: | Viana(@thiago_fiago)也在自己的部落格和推特上寫到: |
19 | Heshima ya sheria, usawa, maadili na nchi kutokuwa na mfungamano na dini: hii ni misingi “pekee” iliyovunjwa katika kutoa pasipoti za kusafiria kwa wachungaji. | 合法性、平等、道德倫理、以及政教分離,這些原則都因為簽發給牧師的特別護照而一一瓦解。 |
20 | Mwendesha mashitaka wa serikali Chico (@chiconob) anaendelea katika msimamo huo huo wa mawazo: | 檢察官Chico(@chiconob)也稟持相同看法: 簽發外交護照給宗教神職代表一事無須再強詞奪理,太難看了! |
21 | Hakuna hoja yenye mashiko kutetea kitendo cha kutoa pasipoti za kusafiria za kidiplomasia kwa viongozi wa kidini. Inachefua mno! | 網路上針對此事件的討論再度將巴西政教分離的議題搬上抬面,雖然憲法確定國家和宗教各自獨立分開,但實際上簽發外交護照給宗教領袖的行為已違背此項原則。 |
22 | Mjadala huo mtandaoni unaurudisha tena mezani mdahalo wa siku nyingi na unaoendelea kuhusu dhana ya serikali kutokuwa na dini nchini Brazili. | 畢竟,我們是要如何理解宗教領袖持有外交護照這件事,與政教分離的基本原則互不違背? |
23 | Ingawa katiba inatenganisha bayana masuala ya utawala wa Serikali na yale ya dini, katika hali halisi utoaji wa pasipoti za kidiplomasia kwa viongozi wa kidini unaonekana wazi kuvunja kanuni hiyo, na tuwe wakweli, inawezekana vipi kiongozi wa kidini kubeba pasipoti ya kidiplomasia bila kuvunja kanuni ya msingi kabisa ya nchi kutokuwa na dini? | |
24 | Kiongozi yeyote anayebeba nyaraka nyeti ya kumwezesha kusafiri kidiplomasia hapaswi, kwa wakati wowote ule, kubeba bendera ya kidini, achilia mbali kuhubiri imani zake za kidini katika nchi ya kigeni. | 無論何時,持有外交護照的人員既然已享有官方外交特權,就不應該再堅 持其宗教神職的身份,也更別說還要在他國傳教了。 |