# | cat | swa |
---|
1 | El ministre de Joventut ugandès afirma que vestir de manera indecent pot incitar a les violacions | Waziri wa Uganda: Wanawake Wasiovaa Mavazi ya Heshima Wanaomba Kubakwa |
2 | Una captura de pantalla de la petició de dimissió del ministre. | Picha ya tamko linalomtaka waziri huyo ajiuzulu. |
3 | Segons unes declaracions del ministre ugandès d'Afers de la Joventut [en], Ronald Kibuule, les dones que vesteixen de manera indecent inciten a la violació i els sospitosos d'haver-les violat haurien de ser alliberats. | Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Vijana wa Uganda Ronald Kibuule, wanawake wanaovaa mawazi yasiyositiri miili yao wanaomba kubakwa, na watuhumiwa wanaodaiwa kuwabaka wanawake waliovaa namna hiyo waachiliwe huru. |
4 | També va dir que, en cas de violació, la policia primer hauria d'esbrinar el tipus de roba que duia la víctima i, si fos indecent, ella també hauria de ser acusada d'incitar al delicte. | Alisema vile vile kuwa katika kesi za ubakaji, polisi wawe wa kwanza kusimamia namna wanawake hao waathirika walivyovaa, na kama wamevaa hovyo, nao washitakiwe kwa kosa la kukaribisha uhalifu. |
5 | Kibuule va fer aquestes declaracions al municipi de Kajara, al districte de Ntungamo, el dissabte 21 de setembre del 2012, quan assistia a un dinar de la Societat d'Estalvis i la Cooperativa de Desenvolupament de la Joventut de Kajara. | Kibuule alitoa matamshi hayo akiwa kwenye halmashauri [kaunti] ya Kajara, wilayani Ntungamo siku ya Jumamosi Septemba 21, 2013 wakati akihudhuria ufunguzi wa Chama cha Ushirika na Akiba cha Vijana wa Kajara. |
6 | Les declaracions van aparèixer al diari ugandès Daily Monitor [en] el 24 de setembre, però a l'article no s'explicava el context en què Kibuule va fer aquest comentari. | Kauli hiyo ilionekana kwenye gazeti la Uganda Daily Monitor la Septemba 24, 2013. Makala hiyo, hata hivyo, haikueleza mukhtadha ambao Kibuule alitoa matamshi hayo. |
7 | El parlament ha demanat la compareixença [en] del ministre per donar explicacions sobre el que va dir aquell dia. | Bunge limemtaka waziri huyo ajieleze bungeni ilikuwaje akatoa matamshi hayo juma lililopita. |
8 | Els internautes ugandesos van respondre amb fúria a aquests comentaris utilitzant l'etiqueta #Kibuule al Twitter. | Raia wa Uganda mtandaoni walijadili matamshi hayo kwa hasira wakitumia alama habari #Kibuule kwenye mtandao wa twitter. |
9 | Els que demanen la seva dimissió utilitzen les etiquetes #KibuuleMustGo (Kibuule ha de marxar) i #KibuuleOut (Kibuule fora). | Wale waliomtaka ajiuzulu wanatumia alama habari #KibuuleMustGo [Kiluule Lazima Ang'oke] na #KibuuleOut [Kibuule Nje]. |
10 | Una petició [en] a Change.org exigeix la seva dimissió: | Tamko lililopo kwenye mtandao wa Change.org linamtaka ajiuzulu: |
11 | Amb aquestes paraules, el senyor Kibuule fomenta la violació de dones segons la seva forma de vestir; exculpa els violadors dels delictes contra les dones que van suposadament lleugeres de roba; i s'assegura que les víctimes de violació no s'atreveixen a anar a la policia per por de ser perseguides per haver estat violades. | Kwa manano haya, Bw. Kibuule anautangaza ubakaji wa wanawake kwa kigezo la mavazi yao; anawahurumia wabakaji kwa makosa yao ya jinai waliyoyafanya kwa wanawake wanaodaiwa kuvaa vibaya na; anahakikisha waathirika wa ubakaji wanapata hofu ya kujitokeza hadharani kwa kuogopa kushitakiwa kwa kubakwa. |
12 | Hauria de renunciar al seu càrrec immediatament perquè és evident que no representa el benestar dels seus electors. | Lazima aachane na msimamo huo haraka sana kwa kuwa ni wazi alichokisema hakiwakilishi ustawi wa wapiga kura wake. |
13 | Rosebell Kagumire (@RosebellK), una periodista online ugandesa, va escriure: | Rosebell Kagumire (@RosebellK), mwandishi wa Uganda mtandaoni, aliandika: |
14 | 4.000 nens són violats al nord d'#uganda cada any, estic segura que #kibuule pensa que és perquè van ser provocadors! | Watoto 4000 kaskazini mwa Uganda wananajisiwa kila mwaka. Nina hakika Kibuule anadhani ni kwa sababu watoto hao walivaa vibaya! |
15 | Idiotes al poder! | Wajinga walio madarakani! |
16 | Linda (@LindaNEK), una empresària ugandesa, va ridiculitzar l'autoritat moral del ministre: | Wandera Samuel (@wandyBlackstig) anatafakari mawazo haya ya Waziri yametokea wapi: |
17 | #Kibuule és moralment incompetent per donar cap opinió significativa sobre aspectes morals, sobretot tenint en compte que és polígam @DailyMonitor | Kibuule anakaa kwenye kochi|anabadilisha badilisha chaneli za runinga | anajikuna sehemu nyeti| anafikiri -> kwamba wasichana waliovaa vimini wabakwe |
18 | Mark Namamanya (@mnamanya), un periodista esportiu, va observar: | Linda (@LindaNEK), mfanyabiashara wa ki-Ganda, alikejeli mamlaka ya kimaadili aliyonayo waziri: |
19 | A la majoria de societats, aquest pallasso de #Kibuule avui dimitiria en una roda de premsa. | Kibuule hana ubavu wa kimaadili kutoa matamshi hayo yanayohusiana na Maadili hasa sote tukijua jamaa ana wake wengi @DailyMonitor |
20 | Malauradament, Uganda no és la majoria de societats. | Mark Namamanya (@mnamanya), mwandishi wa michezo, aliona alibaini: |
21 | Gordon G Ananura (@NgabiranoIV) es va unir a aquells que ridiculitzaven el ministre: | Katika jamii nyingi, mtu anayefanya kituko kama Kibuule angekuwa anafanya mkutano na waandishi wa habari kutangaza kujiuzulu. |
22 | @eshbankwesiga @iDEASUG: Sabia que el ministre #Kibuule era una broma. | Inasikitisha, si moja ya jamii hizo nyingi |
23 | Tot i això, alguns ugandesos com Ibrahim Batambuze (@TheBigPapaa) van donar suport a l'argument del ministre: | Gordon G Ananura (@NgabiranoIV) alijiunga na wale waliokuwa wakimkejeli waziri: Nilijua kuwa Kibuule ni kichekesho |
24 | | Hata hivyo, baadhi ya wa-Ganda kama Ibrahim Batambuze (@TheBigPapaa) waliunga mkono matamshi ya waziri: |
25 | @Mr_Bata_ estic totalment d'acord amb tu. | Ninaungana na wewe kwa asilimia 100. |
26 | Si deixes la porta oberta i et roben, a qui has de culpar de la teva estupidesa? #Kibuule | Kama unaacha milango yako wazi na anakuja jambazi anakuibia, unamlaumu nani kwa ujinga wako? |