# | deu | swa |
---|
1 | GV Face: Geheimes “kubanisches Twitter” der USA | Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba |
2 | Ein geheimer Plan der USA, den Regimewechsel in Kuba mithilfe des Twitter ähnlichen Kurznachrichtendienstes ZunZuneo [en] herbeizuführen, ist nun ins Zentrum der Aufmerksamkeit gerückt, nachdem Nachrichtenberichte bekannt gaben, dass tausende Kubaner unter falschen Vorwänden dazu verleitet worden waren, sich bei dem Dienst anzumelden. | Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo. |
3 | Wird das für digitale Aktivistinnen und Aktivisten weltweit Konsequenzen haben? | Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? |
4 | Einige befürchten, es werde zu noch mehr Misstrauen und der Zensur von Internet und sozialen Medien in ihren jeweiligen Ländern führen. | Wengine wana mashaka gatua hiyo inaweza kusababisha hali ya kutokuaminiana na kufuatiliwa kwa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii katika nchi zao. |
5 | Eine lebhafte Diskussion mit Sana Saleem, Ivan Sigal und Solana Larsen. [Hinweis: Das Video ist auf Englisch.] | Majadiliano ya kina na: Sana Saleem, Ivan Sigal na Solana Larsen. |